Ratiba ya michezo -jamhuri ya muungano tanzania [Shule zote za Msingi na Sekondari ziwe zimefungwa] -Wadhamini Benki zote, Tiggo, Vodacom na wauzaji petroli wote nchini.
DESEMBA [2008] Mashindano ya kupata mabingwa wa TARAFA katika michezo yote itakayochaguliwa. Wadhamini NSSF, PPF, Vyombo vyote vya habari, Zain na Zantel.
JANUARI [2009] Mashindano ya kupata mabingwa wa WILAYA katika michezo yote. Wadhamini Vyombo vyote vya uchukuzi reli na barabara, polisi wa usalama barabarani na sekta ndogo binafsi yote.
FEBRUARI [2009] Mashindano ya kupata mabingwa wa MKOA katika michezo yote. Wadhamini Mashirika yote ya Ndege, Machimbo ya Dhahabu na Almasi na Tanzanite na kadhalika.
MACHI [2009] Mashindano ya kupata mabingwa wa TAIFA katika michezo yote. Mdhamini -SERIKALI KUU: MFUKO WA MAENDELEO YA MICHEZO TANZANIA [MFUMAMITA]
APRILI-JUNI [2009] MAPUMZIKO na mazoezi binafsi kwa wanamichezo wote Tanzania pamoja na kushiriki shughuli za uzalishaji mbali kwenye maeneo yao. Mdhamini mkuu ni SERIKALI KUU: MFUKO WA MAENDELEO YA MICHEZO TANZANIA [MFUMAMITA]
JULAI-AGOSTI [2009] Mazoezi ya Nguvu na Maandalizi na uboreshaji wa mabingwa kufikia viwango vya kimataifa pamoja na ushiriki katika michezo ya majaribio ndani na nje.Wadhamini ni SERIKALI KUU: MFUKO WA MAENDELEO YA MICHEZO TANZANIA [MFUMAMITA]
AGOSTI-OKTOBA [2009] USHIRIKI mashindano mbalimbali nchini, Afrika na ulimwenguni kote. WADHAMINI: ORGANIZERS wa michezo hiyo kote waliko! *SERIKALI KUU: MFUKO WA MAENDELEO YA MICHEZO TANZANIA [MFUMAMITA]
- Mfuko huu utashibishwa na shilingi 10 toka makusanyo yote kwenye vituo vya ndege, mabasi na meli; Shilingi 10 toka kila lita ya peteroli na dizeli; shiligni 10 kutoka kwenye kila nauli ya daladala; pamoja na shilingi milioni 200 toka kila kampuni ya simu na migodi ya dhahabu, almasi na tanzanite nchini. [DONE] NOTE: Ratiba hii itakuwa ikijirudia vivyo hivyo kila mwaka!