Monday, August 11, 2008

Tingatinga likichimbua barabara za maeneo ya stendi kuu ya Mkoa katika harakati ya kulifanya eneo hilo kuvutia zaidi.
Ndio maana Dar jiji wameamua kupiga marufuku vipanya, kwa sababu pamoja na kuamini kuwa halitoshi, bado linalazimishwa kuwa basi kubwa ba lori hapo hapo. Hiki ni kipanya kikiwa maeneo ya VETA kikielekea Muheza nyakati za jioni sana, mizigo inayoonekana ni Baiskeli ambazo ni za wafanyabiashara wa Mkaa, mihogo, maziwa na bidhaa nyingine haswa kutoka eneo la Kilapura, Ngomeni , Mkanyageni na Tanganyika. Wamekuja kwa baiskeli na mizigo hiyo, lakini kurudi wanatumia pesa walizopata kulipa nauli yao na ya baiskeli zao.. kwa raha zao !!
Bango la tiGO lililo eneo la Kwaminchi linalokukaribisha ktk jiji la Tanga
Hii ni bustani iliyo katika shoto la jirani na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga, likiwa limepambwa na saa ya jiji na Tangazo la kampuni ya sementi ya Simba cement ya Tanga.
Shoto la Kwaminchi nyakati za jioni
Stendi ya Mkoa ambayo barabara zako ziko katika ukarabati Mkubwa. Hizi ni jitihada za halamshauri ya jiji kuigeuza tanga inayofahamika na wengi kuwa na sifa za jiji. Sasa ukifika Tanga usiku utadhani umepotea na kwamba hauko Tanga, mitaa ya katikati ya jiji ina ng'aa kwa taa za barabarani zenye kulifanya jiji kuwa na rangi ya kupendeza.



No comments: