Friday, August 15, 2008

KIKAO CHA WAZAZI, 2007(PARENTS MEETING)

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
SHULE YA SEKONDARI TOLEDO
S. L. P. 1852
TANGA
EMAIL: toledosec@yahoo.com




KIKAO CHA WAZAZI 24/12/2007

Kikao kilifunguliwa na Mkuu wa shule saa sita kamili mchana.
Wazazi walipata nafasi ya kutambulishwa uongozi wa shule na taarifa fupi ya shule, taarifa iliyotolewa na Mkuu wa shule.

Baada ya utambulisho, Mkuu wa shule ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho, aliwaeleza wazazi madhumuni ya mkutano , ambapo aliwaeleza wazazi kuwa nia ya kuwaita ni kuwatambulisha aina ya shule na utaratibu wa uendeshaji wa shule hii.
Aliwaeleza wazazi kuwa pamoja na kwamba shule hii inapaswa kuendeshwa na serikali, bado yapo mahitaji ambayo serikali haijaweza kuyatimiza, na hivyo kuwepo na umuhimu wa wazazi kuchangia gharama za uendeshaji.
Baada ya hapo, Mkuu wa shule alimkaribisha Ndugu Mbaraka Pemba ambaye aliwakilisha kamati ya ujenzi na ambaye ni katibu wa kamati hiyo ili kueleza juu ya hatua zilizofikiwa kuhusu ujenzi wa madarasa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2008.

Bwana Pemba aliwaambia wazazi wasiwe na wasiwasi, kwani watoto wao wataingia darasani kama ilivyokusudiwa kutokana na mipango iliyopangwa na kamati ya ujenzi ya shule na ambayo ilipitishwa na kikao cha bodi ya shule pia.

Mipango hiyo ni ya kukusanya michango kama ifuatavyo:-
Wananchi wa kata 4 wanategemewa kuchangia 2500/= kwa kila kaya.
Kila shule ya msingi itachangia 100,000/=, ambapo zipo shule nne hivyo kupata 400,000/=
kila mwanafunzi shule yamsingi atachangia 200/= wanategemea 800,000/= .
Wazazi wa wanafunzi,Toledo Sec. watachangia 23,000 x 300 = 6,900,000 /=

Akasema kuwa pamoja na michango hii ya wazazi, bado haitoshi kuweza kumalizia madarasa sita yanayotakiwa kwa mwaka huu 2008, na hivyo akasema wahisani mbalimbali pamoja na Halmashauri wataombwa kusaidia.

Pia katibu aliwaomba wazazi kukubali kuchangia gharama za kutengeneza madawati kwa ajili ya watoto wao, maana halmashauri ina mzigo mkubwa ambao haitaweza kukamilisha hadi kutoa madawati kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka huu. Hivyo akawaomba kuchangia shlingi 45,000/= kwa kila mtoto ili kununulia madawati hayo.
Dawati @ 45,000 x 160 = 7,520,000 baada ya maelezo hayo, wazazi walianza kuuliza maswali.
SWALI: hivi hakuna sehemu ya kusomea hawa wanafunzi wa kidato cha kwanza bila kujenga haya madarasa mapya? Vipi kuhusu muda wa kulipia Ujenzi?

JIBU: Katibu wa kamati ya ujenzi alijibu swali hilo kwa kusema hakuna sehemu ya kuwaweka wanafunzi hao kwa sasa labda Mkuu wa shule atafute njia zake ili kuwaweka wanafunzi hawa kwa muda kabla madarasa yao hayajakamilika, nakuwaomba wazazi wajitahidi kutoa hizo pesa mapema ili ziweze kusaidia kumaliza ujenzi wa madarasa manne ya kidato cha kwanza 2008.


SWALI: Risiti ni kitu muhimu sana kwa kila pesa, kutakuwa na risiti juu ya hii michango ya Ujenzi na Dawati?

JIBU: Katibu alijibu swali hilo kwa kusema, yeye ataandaa kitabu cha risiti na shule ya Toledo ndio itakayo kusanya hizo pesa na itatoa hizo risiti ambazo ni za kamati ya ujenzi sio risiti za Toledo Sekondari.


SWALI: Kwanini shule imeitwa Toledo?
JIBU: Mkuu wa shule alisema Toledo ni jina lililotokana na urafiki kati ya jiji la Tanga na jiji la Toledo la Marekani kwa hiyo ni katika kuimarisha urafiki kati ya majiji haya mawili.

Pia Mkuu wa shule aliwaomba wazazi washirikiane na shule katika kushughulikia tabia na nidhamu za wanafunzi pamoja na masomo kwa watoto wao. Mkuu wa shule alisema bila nidhamu hakuna maendeleo kielimu. Suala la utoro kwa wanafunzi pia liliongelewa na mkuu wa shule kwa kuomba ushirikiano wa karibu sana na wazazi.

Mkuu wa shule pia aliwaomba wazazi kuwa na uatamaduni wa kuwanunulia watoto wao vitabu kwani vya shule ni vichache sana.

Shule ina upungufu wa waalimu wa somo la Biolojia na Kemia, hivyo ina mpango wa kuajiri mwalimu wa Chemistry/Biology kwani kulikuwa na mwalimu mmoja tu alisema mkuu wa shule, pamoja Katibu Muhtasi.

Michango ya shule

Mkuu wa shule aliwaelezea wazazi juu ya umuhimu wa kuchangia taaluma, ulinzi pamoja na kutoa ada ya shule.
Mkuu wa shule aliwaomba wazazi wawe natabia ya kulipa ada kidogo kidogo kila mwezi ili wasingoje deni kuwa kubwa.

Mkuu wa shule aliwaomba wazazi kulipa Ths.81,000/= au 85,000/=kwa ajili ya ada, sare na michango mbalimbali ya shule ukiwemo wa Mlinzi 10,000/= kwa mwaka na Ths.10,000/- za taaluma kwa mwaka. Fedha hizi zitatolewa kwa awamu, kidogo kidogo ndani ya mwaka.

Mkuu wa shule alieleza kuwa Mchango wa Mlinzi ni kutokana na hali ya usalama ulivyo mbaya katika eneo iliko shule ambapo kumekuwa na matukio mbalimbali ya wizi wa vifaa vya shule toka shule ilipoanza, ikiwepo kuibwa kwa vyoo , milango, bati na vifaa vingine.

Kuhusu mchango wa taaluma, Mkuu wa shule alieleza wazazi kuwa fedha hiyo itatumika kulipa mshahara kwa mwalimu mmoja wa kemia na biolojia, na hesabu, pamoja na katibu muhtasi. Pia mchango huu utatumika kuendeshea mitihani ya majaribio ya kila mara na kulipa waalimu watakaojitolea kufundisha muda wa ziada wanafunzi wenye uelewa wa taratibu (Remedial classes)
Mkuu wa shule alieleza kuwa mahitaji yote hayo yapo katika fomu ya kujiunga, ambayo kila mzazi atapewa.


Wazazi walikubaliana na maelezo hayo kukubali kulipa 23,000/= za ujenzi pamoja na 45,000/= za dawati ili watoto wao wasome, Pamoja na kulipa ada na michango mingine.
Jumla ya wazazi 77 walihudhuria kikao hicho.


Kikao kilifungwa saa saba na robo mchana kwa mkuu wa shule kuwashukuru wazazi kwa uvumilivu wao, na kuwaomba kuwa karibu na utawala wa shule kwa ajili ya maendeleo ya watoto wao.




____________ _______________
MWENYEKITI KATIBU

No comments: