Wednesday, August 6, 2008

MITANDAO YA SIMU



Mitandao ya simu za mkononi sasa si kitu cha ajabu tena, na wala si anasa kama ilivyokuwa ikionekana hapo mwanzo wakati inaingia. Wakati ule Mobitel na Tritel walipokuwa wanauza ''line'' kwa Tsh.60,000/=, na ambapo mtandao ulianza kuwa hadi Ubungo tu, na baadaye miji mikuu ya mikoa. Kwa sasa mitandao inapatikana hadi Kwehungulu na Mng'aro za Lushoto, Lipaya na Kikunja za Ruvuma. Kwa sasa hadi wafanyakazi wa ndani wana mitandao, wala si anasa tena ila muhimu kwa mawasiliano, japo unaweka Tsh 1,000/= kwa mwezi mzima inayotumika kubip tu !
wengine wanatumia pesa nyingi kiasi kwa mwezi, ambazo akitajiwa ametumia kiasi gani mwezi huu anaweza kupata kichaa.!!
Ongezeko la waomba credits nalo limekuwa kubwa sana..ajabu ni kuwa asilimia 90 ya waomba vocha ni wadada!! Kuna mmoja aliniambia kwa siku anakusanya kama elfu kumi hadi ishirini kwa kuomba vocha kwa marafiki..ka-mradi ati!!
Tatizo la udanganyifu kwa kutumia simua mkono nalo ni balaa..utasikia mtu tena kwenye daladala anasema ''niko dar bwana narudi wiki ijayo'' kumbe yuko Ngamiani sokoni, na wengine kutumia simu hizi kutukana wengine. Ni kwa sababu hii tanzania kwa kutumia tume ya mawasiliano inakusudia kuweka utaratibu wa kuthibiti wanunuzi wa line za simu ili kuwa na kumbukumbu zao. wadau mnasemaje, itakubaliana mwendo kasi wa soko huria la biashara?? hebu toa maoni yako!!

No comments: